Ministry of Natural Resources and Tourism Community Based Conservation Training Centre (CBCTC) Likuyu Sekamaganga
Community Based Conservation Training Centre (CBCTC) Likuyu Sekamaganga
LMS
SMIS
Mail
Eng
close
close
Head

BALOZI WA TANZANIA NCHINI ITALY ATEMBELEA BANDA LA MALIASILI.

Balozi2.jpeg Leo tarehe 4.8.2026 Balozi wa Tanzania nchini Italy Mbarouk Nassor Mbarouk ametembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii lililopo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi(Nanenane) yanayoendelea Nzuguni Dodoma na kujionea na kujinza mambo mbalimbali. Katika ziara yake alipata fursa ya kufika katika meza ya Chuo Cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii na kuelezewa mchango wa chuo katika kuishirikisha Jamii juu ya njia mbalimbali za kukabiliana na wanyamapori wakali waharibifu. Pia alifahamishwa juu ya mafunzo ya muda mrefu yanayotolewa na chuo kwa ngazi ya Cheti na Diploma. Chuo Cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii Likuyu Sekamaganga kinashiriki Maonesho haya ambapo watu wanapata fursa ya kujifunza shughuli za chuo pamoja na kuelekezwa udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2026/2027. Karibu katika meza ya Chuo iliyopo katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kwa huduma ya udahili na maelekezo mbalimbali au unaweza kuomba kujiunga na chuo kupitia website au kwa kuwasiliana na Afisa Udahili kwa namba 0738102111.

Balozi1.jpeg

Balozi3.jpeg

Posted in Uncategorized on Aug 06, 2026