NAIBU MTENDAJI MKUU SUMA JKT BRIGEDIA JENERALI SHIJA LUPI ATEMBELEA MEZA YA CHUO CHA MAFUNZO YA UHIFADHI WA MALIASILI KWA JAMII LIKUYU SEKAMAGANGA.
Leo tarehe 3.8.2026 Naibu Mtendaji Mkuu SUMA JKT Brigedia Jenerali Shija Lupi ametembelea meza ya Chuo iliyopo katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii lililopo katika Maonesho ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Nanenane Dodoma.
Amepata nafasi ya kupata taarifa ya mafunzo kwa kozi ya Utalii na Uongozaji Watalii ambayo Udahili wake unaendelea katika Meza ya chuo.
Amefahamu jinsi chuo kinavyoandaa Askari wa wanyama pori wa vijiji na wanavyotumika kutatua changamoto za migogoro ya wanyama pori na wanadamu katika maeneo wanayoishi.
Amefahamishwa jinsi Askari wa wanyama pori wa vijiji wanavyopatikana kwa ajili ya kuletwa katika mafunzo.
Chuo Cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii Likuyu Sekamaganga kinashiriki Maonesho haya Hadi siku ya mwisho tarehe 10.08.2026 hapa viwanja vya Nanenane Dodoma.
Jamii inaombwa kutembelea meza ya Chuo iliyopo katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ili kujifunza mambo mbalimbali kuhusu ushirikishwaji wa Jamii katika Uhifadhi na utatuzi wa migogoro ya wanyama pori na wanadamu .
Udahili wa wanafunzi unaondelea kwa mwaka wa masomo 2026/2027 karibu upate huduma ya udahili au unaweza kufanya kupitia tovuti ya chuo au mawasiliano: 0738102111.

