Naibu Katibu Mkuu (Mifugo)
Dkt. Fabian Magawa Madele atembelea meza ya Chuo Cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii Likuyu Sekamaganga katika viwanja vya maonesho ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi Nzuguni Dodoma (Nanenane) na kupatiwa taarifa ya aina ya mafunzo yanayotolewa chuoni hapo. Pia amepata fursa ya kupata ufafanuzi wa mafunzo ya Askari wa wanyama pori wa vijiji ambayo yanaendelea chuoni na jinsi chuo kinavyoibeba dhana ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii hasa katika mchango wake mkubwa katika kudhibiti wanyama wakali waharibifu. Maonesho haya yanaendelea Hadi tarehe 10.8.2026 katika viwanja hivyo ambapo huduma ya Udahili kwa mwaka wa masomo 2026/2027 inapatikana katika meza ya Chuo inayopatikana katika Banda la wizara ya Maliasili na Utalii.