Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dr. Ashatu Kijaji(Mb) atembelea meza ya Chuo Cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii - CBCTC Likuyu Sekamaganga iliyopo katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii na kupatiwa taarifa ya mafunzo yanayotolewa na chuo hiki.
Licha ya kupatiwa maelezo ya Udahili wa wanafunzi unaondelea kwa mwaka wa masomo 2026/2027 kwa mafunzo ya muda mrefu kwa ngazi ya Cheti na Diploma katika Kozi ya Utalii na Uongozaji watalii Mh. Waziri pia alipewa maelezo ya kina jinsi chuo kinavyoweza kuitafsiri dhana ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii na kuandaa Askari ambao wamekuwa chachu kubwa katika kutatua migogoro ya wanyama pori na wanadamu katika maeneo yenye migongano kati ya wanadamu na wanyamapori. Chuo hiki kimekuwa kitovu Cha kuandaa wataalam wa kudhibiti migongano ya wanyama pori na wanadamu kwa miaka mingi na kuwa msaada mkubwa kwa Jamii zinazokumbwa na changamoto hii.
Karibu katika meza ya Chuo iliyopo katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii lililopo katika Maonesho ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Nanenane Dodoma kwa ajili ya kujifunza na kupata huduma ya Udahili kwa mwaka wa masomo 2026/2027.
Au omba kupitia tovuti ya chuo.
Mawasiliano
0738102111

