Ministry of Natural Resources and Tourism Community Based Conservation Training Centre (CBCTC) Likuyu Sekamaganga
Community Based Conservation Training Centre (CBCTC) Likuyu Sekamaganga
LMS
SMIS
Mail
Eng
close
close
Head

PONGEZI NYINGI ZA MIMINIKA KWA CBCTC LIKUYU SEKAMAGANGA Nzuguni Dodoma. NNN.jpeg Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Chande, amekipongeza Chuo Cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii Likuyu Sekamaganga kwa kuwa muhimili wa utatuzi wa migogoro ya wanyama pori na wanadamu. Ameyasema hayo alipotembelea meza ya Chuo iliyopo katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii lililopo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nanenane) yanayoendelea jijini Dodoma. Chuo Cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii Likuyu Sekamaganga kinatoa mafunzo ya kukabiliana na wanyamapori wakali waharibifu kwa Jamii ili kupunguza changamoto hizi kwa Jamii ambazo zimepakana na hifadhi mito,mabwawa na maziwa. Pia chuo kinatoa mafunzo ya Utalii na Uongozaji Watalii ambayo Udahili wake unaendelea katika Meza ya Chuo iliyopo katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii na kupitia tovuti ya chuo na kwa njia ya Whatsapp namba 0738102111.

Posted in Uncategorized on Aug 07, 2026